Breaking News

Shonga, huyooO Ureno

Justin Shonga, mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini inaelezwa kuwa yupo mbioni kujiunga na Klabu ya CS Maritimo ya nchini Ureno, hiyo ni baada ya kushindwana na klabu ya Simba.

Shonga raia wa Zambia, inasemakana ameshindwana na klabu ya Simba kwa kuwa dau lake la usajili lipo juu sana. 

Inatajwa kuwa thamani yake sokoni ni Euro 600,000 (zaidi ya Sh bilioni moja), sasa huenda hiyo ndio ilikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba ambayo ilikuwa imeshakubali kumlipa mshahara wa Sh mil 34 kwa mwezi, kwa mujibu wa watu wake wa karibu.

Hivyo basi mazungumzo na na klabu ya Maritimo yameonekana kufikia muhafaka na wakala wake pia na klabu yake ya Orlando Pirates.

No comments