Martial aweka historia tangu kuondoka kwa Feguson 2013
Manchester,England. M shambuliaji wa Manchester United, jana aliandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja, ‘hat trick’ tangu aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson kuondoka mwaka 2013 baada ya kuiongoza United kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sheffield United katika Uwanja wa Old Trafford.
Tangu Robin Van Persie alipofanya hivyo dhidi ya Aston Villa mwaka 2013 ambao ndio ulikuwa wa mwisho kwa Ferguson kuinoa timu hiyo, hakuna mchezaji mwingine wa United aliyeweza kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja kama alivyofanya Martial jana.
No comments