Upamecano aziweka vitani Manchester United na City
Klabu ya Manchester United na Manchester City zote kwa ujumla zimeonesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kimataifa wa Ufaransa, Dayot Upamecano anayeichezea klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa na msimu bora wa 2019/2020 na kutajwa kua ni mmoja wa mabeki bora barani Ulaya na kufanya Ole Gunnar Solskjaer na Pep Guardiola kuwania saini yake.
No comments