Pogba afunguka mwanzo alikua mshabiki wa Arsenal
Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amefunga na kusema kuwa, kipindi akiwa mdogo yeye alikuwa ni shabiki mkubwa wa klabu ya Arsenal kutokana na mtu aliyekuwa akimfuatilia sana "Thierry Henry" mfaransa mwenzake.
Pogba alijiunga na United kutoka Le Havre akiwa na miaka 16 mwaka 2009, kabla ya kwenda Juventus 2012 na baadae kurejea UTD miaka 4 baadae kwa rekodi ya dunia ya uhamisho wake.
Mfungaji wa muda wote wa Arsenal, Henry ni miongoni mwa watu waliotajwa na Pogba kuwa huwa anapenda kuwafuatilia sana wengine ni Ronaldinho, Ronaldo na Zinedine Zidane. Pogba anasema. "Nitakuwa mkweli. Mwanzoni, Mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa ARSENAL hiyo ni kwasababu ya Wachezaji wote wa UFARANSA unaowajua walikua wanaichezea Arsenal." alitanabaisha Pogba kupitia United's official podcast.
"Mimi na kaka yangu tulikuwa mashabaki wa ARSENAL, lakini kaka yangu mwingine ndiye aliyekuwa shabiki wa Man UTD. "Siwezi kusema chochote lakini, Nilikuwa nampenda Henry na kwasababu yake Mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa ARSENAL. Baadae nilibadili na kumfuata kaka yangu mwingine. Niliiacha Arsenal, na kujiunga na kaka yangu aliyekuwa mshabiki wa Man United." Alisema Pogba

No comments