Breaking News

Ligi kuu Ufaransa kurudi Juni 3

Ufaransa inafikiria kuanza tena kwa ligue 1 mnamo mwezi Juni 3 au Juni 17, Gazeti la michezo la kila siku la Ufaransa la "L’Equipe" limeripoti.

Michezo yote Ufaransa ilisitishwa kwa muda usiojulikana mwezi uliopita kwa sababu ya janga la COVID-19. Mnamo Jumatatu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliongeza siku za watu kuwa ndani (self isolation) nchini hadi Mei 11.

Taarifa zinadai kuwa ikiwa msimu utaanza tena Juni 17 timu zingelazimika kucheza kila baada ya siku tatu ili kuhakikisha kampeni hizo zinamalizika mwezi Julai 25, .

No comments