Breaking News

Ligi kuu Uholanzi imefuta msimu 2019/2020 na hakutakuwa na bingwa

Baada ya waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte kusimamisha michezo hususani mchezo wa soka la kulipwa mpaka mwezi Septemba 2020, chama cha soka nchini Uholanzi kimeamua kuufuta kabisa msimu wa ligi 2019/2020 na kuamua mambo yafuatayo:-

1: Hakuna timu itakayoshuka daraja
2: Hakuna timu itakayopanda daraja
3: Vinara Ajax hawatotwaa taji msimu huu.

A: Ajax wataenda katika raundi ya mwisho ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

B: AZ wataenda katika raundi ya pili ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

C: Feyenoord wataingia hatua ya makundi ya Europa Ligi.

D: PSV wataenda katika raundi ya tatu ya kufuzu kombe la Europa.

E: Willem II wataenda kwenye raundi ya pili ya kufuzu kombe la Europa.

1: Timu 16 zilipiga kura kuwepo na timu kupanda na kushuka daraja.

2: Timu 9 zimepiga kura kutokuwepo kwa kushuka na kupanda daraja.

3: Timu 9 zingine hazikupiga kura na kuamua kuwaachia chama cha soka kufanya maamuzi.

Hivyo basi imepelekea ligi kuu nchini Uholanzi Eridivise kuwa ndio ligi ya kwanza barani ulaya kufutwa kwa sababu ya janga la Corona.

No comments