Breaking News

Juve wameelekeza nguvu kwa Kane


Juventus sasa wanaelekeza nguvu zao kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Tottenham Harry Kane. (Corriere dello Sport - in Italian)
Real Madrid wametoka kwenye kinyang'anyiro cha kumnyakua Harry Kane kutokana na athari za kiuchumi zinazosababishwa na virusi vya corona. (Mail)

Real pia wanafikiria kuwauza wachezaji mpaka sita wa kikosi cha kwanza, akiwemo winga wa Wales Gareth Bale, 30 na kiungo James Rodriguez, 28. (AS)

Paris St-Germain wanaandaa mkataba mpya mpaka mwaka 2025 kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazili Neymar. Neymar, 28 atapata kitita cha euro milioni 38 (pauni milioni 33) kwa mwaka. (Sport - in Spanish)

Arsenal na Manchester United wanafikiria kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele,22. (Sport - in Spanish)

No comments