Mechi ya Man City na Arsenal yahairishwa kuhofia virusi vya Corona

Mchezo uliopangwa uchezwa leo usiku kati ya Manchester City na Arsenal umeahirishwa.

Hatua hii imekuja baada ya kubainika kuwa wafanyakazi na wachezaji wa Arsenal walishikana mikono na mmiliki wa Olympiacos na Nottingham Forest Evangelos Marinakis ambaye amethibitishwa kuathirika na virusi vya Corona, katika mchezo wa Europa League uliochezwa siku kadhaa zilizopita.

Pamoja na mchezo huo kuhairishwa, lakini pia wachezaji na wafanyakazi wa Arsenal wamepewa agizo la kujifungia ndani kwa siku 14 kama inavyoshauriwa na watabibu. .

Wakati huo huo, mchezo wa Europa League kati ya Manchester United vs Lask utachezwa bila mashabiki, kama ilivyo kwa michezo mingine ya Europa League na UCL. 

No comments