Kaizer Chiefs yaingia kwenye anga za FIFA


Baada ya usajili wa kiungo wa kimataifa wa Madagascar , Andriamirado 'Dax' Andrianarimanana klabu ya Kaizer Chiefs wameingia kwenye vita dhidi ya FIFA 

Shirikisho la Soka Duniani limemfungia kiungo huyo wa miamba wa Soweto kwa muda wa miezi minne baada ya kuhamia Kaizer Chiefs kutokea Fosa Juniors.

Juniors walepeleka malalamiko yao FIFA baada ya uhamisho wa kiungo huyo kwenda Amakhosi ( Kaizer Chiefs ) mwaka 2018, kesi ambayo iliyopita wameshinda. 

“ Chiefs wanatakiwa kufungiwa kusajili wachezaji kitaifa na kimataifa kwa misimu miwili mfululizo “ Taarifa ya FIFA imesema hivyo

Amakhosi walimsajili kiungo huyo kwa uhamisho huru baada ya mchezaji kudai kwamba hana mkataba na Fosa Junior. Na matokeo yake Kaizer Chiefs wamefungiwa kusajili na mchezaji pia ameadhibiwa kifungo cha miezi minne kutocheza kandanda kwa udanganyifu wake kuhusu mkataba 

Chiefs wana siku 21 kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo katika Mahakama ya usuluhishi ya Michezo ( CAS )

No comments