Viera siku za kubaki Nice zinahesabika

Klabu ya soka ya Nice ipo mbioni kumtimua kazi legendari wa timu ya Arsenal, Patrie Viera kutokana na matokeo mabovu anayoendelea kuyapata.

Vieira huwenda akatimuliwa baada ya kuiyongoza klabu hiyo inayoshiriki Ligue 1, tangu mwezi Juni 2018.

Usiku wa jana Nice ilikubali kipigo cha mabao 3–2 dhidi ya Le Mans timu inyoshika nafasi ya 18 kwenye Ligi daraja la Pili na hivyo kutupwa nje ya Kombe la Coupe de La League.

Mechi 6 zilizopita za Nice: (Ushindi 0, kufungwa 5, Sare 1)
❌ vs Le Mans
❌ vs Strasbourg
❌ vs PSG
❌ vs Nantes
⛔ vs Lille
❌ vs Monaco

Mechi ya wikendi hii ni mhimu kwa kocha Patrick Vieira kushinda na wataikaribisha Reims inayoshika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi.

No comments