Breaking News

Bayern wameweka rehani kibarua cha Pochettino

London, England . Mauricio Pochettino ameweka rehani kibarua chake baada ya Tottenham Hotspurs kufungwa mabao 7-2 dhidi ya Bayern Munich.
Hii ni mara ya kwanza Spurs kupata matokeo mabaya baada ya kupita miaka 137 katika historia ya klabu hiyo.
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino alisema dakika 45 za kipindi cha pili zilikuwa ngumu kwao baada ya kucheza vyema dakika 30 za mwanzo.
Pochettino alidai amepokea matokeo hayo kiume. Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Serge Gnabry alifunga mabao manne katika mchezo huo.

No comments