Breaking News

CR7 ameweka rekodi nyingine Juve

Turin, Italia. Cristiano Ronaldo ameweka rekodi nyingine ya ufungaji katika Ligi ya Mabingwa baada ya kufunga dhidi ya Bayer Leverkusen usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo alifunga bao dakika 88, katika ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Juventus katika mchezo wa Kundi D uliofanyika kwenye Uwanja Allianz.
Bao hilo la Ronaldo linamfanya nyota huyo kufunga dhidi ya timu 33 katika Ligi ya Mabingwa akifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Raul.
Ronaldo haiwezi kujisahau kwa rekodi hiyo kwa sababu mshindani wake mkubwa Lionel Messi naye amezifunga timu 32 katika mashindano hayo.

No comments