Breaking News

Pogba & Neymar Mambo yamegonga mwamba


Ndoto ya mshambuliaji Neymar kuondoka Paris Saint-Germain msimu huu imeshindikana baada ya dirisha la usajili majira ya kiangazi kufungwa usiku wa kuamkia leo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, inadaiwa alikuwa tayari kuongezea Paund 17.7milioni ili kuhakikisha anarejea Hispania hasa kwenye klabu yake ya zamani ya FC Barcelona licha ya kuwa Real Madrid nao walionyesha nia ya kumsajili.
Akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa itamlazimu kurejea kwenye mipango ya kikosi cha Thomas Tuchel ambacho tangu msimu huu kuanza hajacheza mchezo hata mmoja.
Mbali na Neymar, kuna majina mengine makubwa ambayo na yenyewe usajili wao umegonga mwamba majira haya ya usajili, akiwemo Paul Pogba, Christian Eriksen, Bruno Fernandes na Ivan Rakitic wote wamesalia kwenye klabu zao.
Pogba alikuwa akiwindwa na Real Madrid huku pia akihusishwa kurejea Juventus, Eriksen ambaye anataka kukabilina na changamoto mpya za soka kwingine alikuwa akihusishwa na vigogo vya barani humo, Real na PSG.

No comments