Rungu ya Bodi ya Ligi yamlima Mwinyi Zahera
Kocha Mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera ametangazwa kuadhibiwa kwa kufungiwa mechi 3 kwa kejeli kwa bodi ya Ligi na faini ya Tsh 500,000/= kwa kuvaa mavazi yasiyokuwa ya kinidhamu (kaptura/pensi/bukta) isiyokuwa sare ya timu wakati wa game ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting iliyomalizika kwa Yanga kufungwa 1-0.
Hivi karibuni Bodi ya Ligi iliboresha sheria zake ikiwemo sheria ya mavazi kwa makocha ambao mara nyingi wanaruhusiwa kuvaa mavazi nje ya uniform za benchi la ufundi kama watapenda kufanya hivyo, Zahera angeweza kusalimika kama nguo alizokuwa amevaa kama zingekuwa sare za benchi la ufundi kama ilivyokuwa kwa Ruvu Shooting
No comments