Breaking News

Taifa Stars walazimisha sare


Bujumbura . Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kulazimisha sare 1-1 ugenini dhidi ya Burundi shukrani kwa bao la mshambuliaji Saimon Msuva kwenye Uwanja wa Intwari jijini Bujumbura.
Msuva alifunga bao hilo la kusawazisha akitumia vizuri uzembe wa kukosa maelewano kwa kipa wa Burundi, Jonathan Nahimana na beki wake katika dakika 84.
Wenyeji Burundi walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika baada ya makosa ya mebeki wa Tanzania kushindwa kuzia krosi iliyomkuta Amissi Cedric aliyemtoka Gadiel Michael na kupiga shuti lililomshinda kipa Juma Kaseja na kujaa wavuni.
Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kusonga mbele iwapo watapata suluhu katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar es Salaam Septemba 8, katika kuwania kutinga hatua ya makundi ya mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.

No comments