Licha ya kupigwa faini lakini bado yumo
MWANZA. PAMOJA na kupewa adhabu kwa kushindwa kuvaa mavazi nadhifu akiwa kwenye benchi lakini kocha huyo wa Yanga, Mwinyi Zahera hajaacha kuvaa mavazi yake ambapo kwenye mechi yao ya kirafiki dhidi ya Pamba amevaa mavazi yake ya siku zote, pensi na fulana.
Yanga inacheza mechi hiyo uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni moja ya maandalizi yao kuelekea mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco itakayochezwa Septemba 14 uwanja wa Taifa.
Zahera amepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa hilo wakati timu yake ilipocheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambayo walipoteza kwa bao 1-0.
Leo Jumamosi, ametinga pensi yake ile ile iliyompelekea kupewa adhabu na bodi ya ligi katika mchezo unaoendelea hivi sasa ambao ni wa kirafiki.
Wakati Zahera akiwa amekitinga pensi hiyo, Kocha mkuu wa Pamba Muhibu Kanu ameulamba suti yenye rangi nyeusi na tai nyekundu inayomuonyesha akiwa kwenye hali ile inayotambulika kama unadhifu

No comments