Breaking News

Azam wameweka mzigo wa kutosha kwenye Udhamini

Dar es Salaam . Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya takribani Shilingi 6.3 bilioni kwa haki za matangazo ya Kombe la FA na mechi za timu ya taifa.
Mikataba hiyo miwili imesainiwa leo katika makamo makuu ya Kampuni ya Azam Media yaliyopo Tabata jijini Dares Salaam.
Mkataba wa udhamini wa mashindano ya Kombe la FA ni wa miaka minne na utakuwa na thamani ya Shilingi 4.5 bilioni ambao utaanza msimu huu baada ya ule wa mwanzo kumalizika.

No comments