Breaking News

VAR ilijichanganya kuamua goli lililokataliwa la Sheffield United dhidi ya Aston villa

Imeelezwa kuwa refa wa mchezo uliopigwa Juni 17, kati ya Aston Villa dhidi ya Sheffield United uliichanganya teknolojia ya goli pamoja na macho ya mwamuzi wa kati.

Kwenye mchezo huo Sheffield United ilipata bao ambalo liliamuliwa na VAR kuwa sio goli kipindi cha kwanza ambalo liliokolewa na mlinda mlango wa Aston Villa Orjan Nyland ambaye aliingia nao ndani ya goli.

Taarifa zinaeleza kuwa kamera saba ndani ya uwanja zilishindwa kuelewa usawa wa mlinda mlango,mabeki wake pamoja na eneo la lango la goli huku ikielezwa pia hata mwamuzi wa kati alichanganyikiwa.

Michael Oliver aliyekuwa mwamuzi wa kati alitazama teknolojia ya goli haikumpa jibu sahihi jambo ambalo Sheffield United walilamikia suala hilo baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu hizo kutoshana bila kufungana.

No comments