Utamu VPL kurejea tena Juni 13
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo mapema hii leo amesema ya kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kutimua vumbi kuanzia Juni 13 mwaka huu baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na janga la virusi vya corona.
Mbali na hayo atanabaisha kuwa ratiba kamili kutolewa Jumapili ya wiki hii tarehe 31.
No comments