Chelsea wapeleka majeshi kwa Jesus Corona
LONDON ENGLAND. SIKIA hii. Chelsea inaripotiwa kumtolea macho staa wa FC Porto, Jesus Corona kuwa litakuwa chaguo sahihi kwao kuliko Jadon Sancho.
Corona, ambaye ana uwezo wa kucheza kiungo wa pembeni au beki wa pembeni, amefunga mabao mawili na kuasisti mara 17 kwenye michuano yote msimu huu aliyokipiga kwenye kikosi hicho cha Primeira Liga.
Kocha wa Chelsea, Frank Lampard awali mpango wake ulikuwa kumnasa staa wa Borussia Dortmund, Sancho, lakini baada ya kuona Manchester United wamepiga hatua kubwa kwenye mbio za kumfukuzia Mwingereza huyo, amebadili mawazo na sasa kumgeukia Corona wa FC Porto.
No comments