Kante aacha kufanya mazoezi


LONDON ENGLAND. Kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante ameruhusiwa kutofanya mazoezi na wenzake baada ya kuingiwa na hofu ya kuambukizwa virusi vya corona.
Kante alifanya mazoezi na wenzake Jumanne iliyopita, wakati Chelsea ilipokuwa moja ya timu zilizoanza mazoezi kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu England.
Lakini, hakuonekana katika mazoezi ya Jumatano akiwa amepewa ruhusa na kocha Frank Lampard. Haifahamiki ni lini Mfaransa huyo atarejea kuungana na wenzake.
Uamuzi wa Kante umekuja baada ya kuripotiwa kwamba, kuna watu sita wamekutwa na maambukizi ya corona katika awamu ya kwanza ya Ligi Kuu England, kuwapima wachezaji pamoja na maofisa wa klabu kabla ya ligi hiyo kuanza upya

No comments