JPM arudisha michezo kuanzia June Mosi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameruhusu michezo yote iliyokuwa imesitishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona ikiwemo Ligi kuu ya Tanzania Bara, Ligi Daraja la kwanza na ligi ya daraja la pili na pia hata michezo mingine iendelee kuanzia tarehe 01/06/2020.
"Kwa trend tuliyoiona sina hakika kama kuna mwanamichezo yeyote aliyefariki kwa Virusi vya Corona na michezo iko mingi kila mmoja ana michezo yake, lakini michezo inasaidia kupambana na janga ili, kwahiyo kuanzia June 1, 2020 michezo irudi kama kawaida" Rais Magufuli.
Ameitaka wizara ya afya na wizara ya michezo kushirikiana ili kuweka utaratibu wa tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona wakati wa mechi na michezo mingine.
Post Comment
No comments