Breaking News

Ndombele katika mipango ya Barcelona kuimalisha safu ya kiungo

Barcelona wanataka kumsajili kiungo wa Tottenham Hotspurs, Tanguy Ndombele na wametoa ofa ya wachezaji wawili kwa Tottenham Hotspurs kama sehemu ya dili hilo.

Barca wanataka kuongeza nguvu kwenye safu yao ya kiungo na wanamtaka Mfaransa huyo licha ya kuwa na msimu mbaya ndani ya Spurs. 

Mabingwa hao wa La Liga hawatoweza kutoa fedha inayohitajika na Spurs kutokana na uchumi kuyumba uliosababishwa na Virusi vya Corona, kwahiyo wamewapa Spurs nafasi ya kuwasajili beki wa kati Samuel Umtiti na beki wa kulia Nelson Semedo.

No comments