Breaking News

Simba, Yanga zatinga nusu fainali


SIMBA SC

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imemkaribisha kiungo wake mpya Luis Miquissone kwa ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco, Sharaf Shiboub na Ibrahimu Ajibu huku lile la kufutia machozi la Zimamoto likifungwa na Hamad Hamad.
Simba watakutana na Azam Fc mechi inayofuata.

YANGA SC

Huku majirani zao yanga wakiibuka na ushindi wa magoli mawili dhidi ya Jamhuri FC. Magoli yakiwekwa wavuni na Adeyum Ahmed pamoja Mohamed Issa.
Yanga watakutana na Mtibwa katika mechi inayofuata.

No comments