Atletico yaizamisha Barcelona Spanish Super Cup

Spanish Super Cup

Atlético de Madrid yaichapa Barcelona kwa idadi ya magoli matatu(3) kwa mawili(2), magoli yaliwekwa kimiani na Koke, Morata na Correa kwa upande wa Atletico na Messi & Griezman. Huku mabao mawili yakikataliwa kwa mfumo wa VAR yaliyofungwa na Messi pamoja na Pique.

Baada ya Atletico Madrid kuitungua Barcelona 3-2 na Jana Real Madrid kuitungua Valencia 3-1 sasa fainali itapigwa baina ya Real Madrid Vs Atletico Madrid tarehe 12.01.2020, hivyo basi fainali itaikutanisha derby ya madrid.

Hizi ni klabu mbili ambazo hazikutwaa taji lolote la ndani ( Nchini Hispania ) wakiwa wamenufaika na mabadiliko ya muundo wa kucheza Spanish Super Cup. Mabingwa wa kombe la Mfalme walikuwa Valencia na Mabingwa wa La Liga walikuwa Barcelona. Kandanda raha sana.

Nani atakuwa Bingwa wa Spanish Super Cup tarehe 12 .01 .2020 ???                                MADRID DERBY

No comments