Boubakary Soumare wa Lille aziingiza vitani Man u, Arsenal na Chelsea

Tetesi za Usajili

Klabu tatu za ligi kuu ya  Uingereza Arsenal, Chelsea na Manchester United zinapigana vikumbo kuiwania saini ya kiungo wa Lille Boubakary Soumare, ambaye kuna uwezekano mkubwa akauzwa Januari hii ( Sky Sports )

Klabu mbili kutoka Hispania Real Madrid na Valencia nazo zimeripotiwa kutaka saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa chini ya miaka 21 ambaye alitua Lille kutoka PSG kwa uhamisho huru uliofanywa na Mkurugenzi wa Michezo wa Lille Luis Campos

Dili linaweza kufanywa katika siku 10 zijazo lakini Lille wangetamani kuwa naye mpaka siku ambayo watacheza mechi ya Ligi dhidi ya PSG  Januari 26 .

No comments