Breaking News

Super Frank leo ataweza kuendeleza rekodi ya kutopoteza kwenye ardhi ya Hispania?

Dondoo 5 kuelekea mchezo wa Valencia na Chelsea leo katika usiku wa ulaya.


  • Katika mechi 7 za Uefa zilizopita, Valencia wameshinda mechi 1 tu dhidi ya Chelsea (W1 D3 L3), wakishinda mechi hiyo darajani msimu huu.
  • Katika mashindano ya Ulaya (European Competition), Valencia imecheza na timu 9 kutoka Uingereza wakiwa nyumbani na wakifanikiwa kuzifunga timu 7 katika ya 9 (Arsenal, Leeds Utd, Liverpool, Man City, Man Utd, Nottingham Forest, na Stoke City), lakini wakiangukia pua timu 2 (Chelsea - mechi 3), na (West Bromwich Albion - mechi 1).
  • Katika mechi 11 za Uefa walizocheza Chelsea huko Spain, Chelsea wamepoteza mechi moja tu (W3 D7 L1), wakifungwa na Barcelona mnamo Machi 2018 dhidi ya Barcelona 3-0 Hatua ya 16 bora
  • Chelsea wanatarajia kushinda mechi yao ya tatu mfululizo ya Uefa wakiwa Ugenini na endapo wakishinda itakuwa ni kwa mara ya kwanza tangu waliposhinda mechi 5 mfululizo ugenini msimu wa 2003/04.
  • Valencia ni moja ya timu 5 ambazo hazijafunga goli katika kipindi cha kwanza mashindano ya Uefa msinu huu, magoli sita ya Valencia msimu huu (Uefa) yamefugwa kipindi cha pili.

No comments