Breaking News

Sneijder asema angejituma angekua daraja moja na Ronaldo pamoja na Messi


Wesley Sneijder anaamini kwamba angeweza kutajwa katika daraja moja na Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi kama angekuwa amejituma zaidi.

Sneijder ambaye amewahi kukipiga katika klabu kadhaa zikiwemo Ajax, Real Madrid, Inter Milan , Galatasaray na Nice ametwaa mataji ya Ligi pamoja UEFA mwaka 2010.

“ Niwe mkweli na nikiri kwamba ningeweza kutajwa katika daraja moja na Ronaldo pamoja na Messi kama ningejituma kwa asilimia 100, najua hilo . Lakini sikutaka kufanya hivyo na sina majuto . Sio kwamba sikuwa na uwezo bali sikutaka tu “.

No comments