Rakitic hana furaha na Barcelona toka ujio wa De Jong
Ivan Rakitic ameongea kuhusu kukosekana kwa muda wa kutosha wa kucheza kikosi cha Barcelona msimu huu mpaka sasa. Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia alikuwa kwenye kikosi cha kwanza msimu uliopita cha Ernesto Valverde lakini msimu huu kumekuwa na ugumu hasa baada ya ujio wa Frenkie De Jong aliesajiliwa kutoka Ajax Amsterdam ya Uholanzi.
“ Mtu unapataje raha? Ni kwa kucheza mpira. Ni kama ninavyosema muda wote. Mtoto wangu mdogo wa kike unadhani huwa anajisikiaje ukichukua mdoli wake? Anajisikia vibaya. Wamechukua mpira wangu, najisikia vibaya. Naonesha hisia zangu. Pindi ukiwa muda wa kulia, hakuna tatizo, pindi ukiwa muda wa kusherehekea, nitakuwa wa kwanza kufanya hivyo “
“ Naelewa na naheshimu uamuzi wa kocha, wa klabu au chochote kile lakini ukweli ni kwamba nimejitoa kikamilifu kwa kila kitu katika kipindi cha miaka mitano na nusu niliyokuwa hapa na ninachohitaji ni kuendelea kufanya hivyo tena na kujisikia vizuri.”
“ Hilo ndio jambo muhimu kwangu. Unajisikia vizuri pale tu unapocheza, nina miaka 31 sio 38 , kiukweli najisikia nipo kwenye wakati mzuri sana sasa hivi wa kucheza kandanda.”
No comments