Mbaye Diagne aadhibiwa na Club Bruges kwa kukosa penalty dhidi ya PSG
Straika wa kimataifa wa Senegal Mbaye Diagne ameondolewa kikosini kwa mechi ya wikiendi hii na kupigwa faini na klabu yake ya Club Bruges kwasababu ya kukosa penati kwenye mechi ya UEFA dhidi ya PSG ambayo walipoteza kwa bao 1-0.
Kocha wa Club Bruges , Philippe Clement ameelezea adhabu hiyo ni kwasababu Hanas Vanaken ndiye aliyeteuliwa kupiga pigaji penati rasmi na sio Diagne.
Diagne aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo alichezewa faulo kwenye eneo hatari iliyopelekea kutolewa mkwaju wa penalty, na ikatokea kutoelewana nani apige ndipo diagne alipoamua kupokonya mpira na kupiga ila hata hivyo iliokolewa kirahisi na golikipa wa PSG, Keylor Navas.
“ Hatocheza katika mechi yetu ya Ligi dhidi ya Antwerp siku ya Jumapili. Na nitaamua katika wiki zijazo au miezi ijayo lini atarudi kwenye timu na pia kutakuwa ba adhabu kubwa ya kifedha “
No comments