Breaking News

Emoji yamponza B. Silva

Bernardo kuikosa Chelsea

Bernardo Silva, kiungo wa Manchester City, amefungiwa mechi  moja na Chama cha Soka Uingereza kufuatia posti yake iliyoashiria ubaguzi wa rangi kwa mchezaji mwenzake, Benjamin Mendy wa Man City.

Na pia amepigwa faini ya kiasi cha Pauni 50,000 na kwa adhabu hiyo ataikosa mechi ijayo ya Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa katika dimba la Etihad .

No comments