Mbivu na Mbichi Kutambulika baada ya dakika 90 leo VPL
Baada ya viwanja Mbalimbali kuwaka moto kwa siku ya jana ... leo tena ni zamu ya Mbeya pamoja na Tanga. Ambapo pata shika nguo kuchanika baina ya :
Mbeya City VS Biashara united Pale Jijini Mbeya
Na Coastal Union VS Mwadui pale Jijini Tanga
Mechi zote hizi Zitachezwa Majira ya 10:00 Jioni. Je nani Kumkalisha mwenzake.. Mbeya City anaweza kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kama ilivyo Kawaida yake au Biashara Anenda Kupindua meza. Na je Coastal Union Ataweza kumgaragarza Mwadui FC wamiliki wa migodi hawa pale tanga ? Au Wazee wa Almasi wataendelea kung'ara Ugenini ? Basi Majibu Ya yote Haya Yatapatikana Baada ya Dakika 90 za michezo yote Mikali ya Ligi kuu.
cc : Nurdinmohamed.com & muziktz.com
Post Comment
No comments