PSG yaweks mzigo kwa Aubameyang
PARIS, UFARANSA. NDO hivyo. Matajiri wa Paris Saint-Germain wameripotiwa kuanzisha mazungumzo na Arsenal kwa ajili ya kumnyakua straika, Pierre-Emerick Aubameyang.
Barcelona na Real Madrid ni miongoni mwa klabu zinazohitaji saini ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambapo wanaamini thamani yake itashuka kutokana na umri wake, muda wa mkataba uliobaki na janga la corona.
Mabingwa hao wa Ligue 1 wameandaa Euro 38 milioni kwa ajili ya kumnasa Aubameyang, mkwanja ambao wanaamini kabisa hauwezi kukataliwa na Arsenal.
No comments