Breaking News

Giggs alewa na mavituz ya Bruno


MANCHESTER, ENGLAND . JAMAA anajua! Ryan Giggs ameibuka na kummwagia sifa kiungo mpya wa Manchester United.
Fernandes, 25, amekuwa kwenye kiwango bora tangu aliponaswa na Man United kwa Pauni 47 milioni akitokea Sporting Lisbon kwenye dirisha la usajili wa Januari.
Amefunga mabao mawili na kuasisti mara tatu kwenye Ligi Kuu England na alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Februari, huku akifunga mara moja na kuasisti katika Europa League.
Ubora wa Fernandes umefanya Man United kucheza mechi 11 za michuano yote bila ya kupoteza kabla ya soka kusimamishwa kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.
“Unaweza kuwasema watu kama Cantona, Van Persie…. sitaki kumlinganisha na hao, lakini yeye ni moja wa wachezaji ambao uwepo wake kwenye timu umepandisha viwango vya wachezaji wengine.

No comments