Samatta aweka historia Wembley, Man city Bingwa
LONDON, ENGLAND.
INAWEZEKANA Aston Villa imekosa ubingwa wa Kombe la Ligi, lakini Watanzania wengi wanasema potelea mbali maadam nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunga bao katika pambano hilo kwao ni raha tu.
Katika mechi ya jana iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley, Aston Villa ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Man City na kupoteza nafasi ya kutwaa taji la michuano hiyo, huku Samatta akiandika historia ya kwa Mtanzania wa kwanza kufunga bao katika Uwanja huo.
Post Comment
No comments