EPL bado mambo magumu!!
Kufuatia tishio la virusi vya corona, kuna uwezekano mkubwa wa ligi kuu ya England kuishia hapa kwa sababu hakuna uhakika kama maradhi haya yataisha hivi karibuni.
Kutokana na hilo, bodi ya ligi hiyo inafikiria kujipanga kwa msimu ujao kwa kuandaa mpango mkakati maalumu utakaopunguza machungu kwa vilabu vyote, angalau!
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, bodi ya ligi inataka kutangaza kusitishwa kabisa kwa msimu na kuikabidhi Liverpool ubingwa.
Lakini hata hivyo, hakutakuwa na timu itakayoshuka daraja, hivyo klabu yetu pendwa ya Aston Villa itabaki salama.
Hii itaviumiza vilabu vya daraja la kwanza ambavyo vinapambania kupanda ligi kuu, kuepuka hilo, bodi ya ligi inataka kuongeza idadi ya timu msimu ujao, hadi 22.
Hii ina maana kwamba timu mbili zitapanda kutoka daraja la kwanza, na kuungana na 20 za msimu huu ambazo zitabaki zote.
Watakaoumia na mpango huu ni zile timu zingine nne za daraja la kwanza ambazo huingia kwenye mchujo kuwania nafasi moja ya kupanda, kwani hakutakuwa na mechi za mchujo kabisa.
Mara ya mwisho EPL kuwa na timu 22 ilikuwa msimu wa 1994/95.
Bodi ya ligi pia inataka kushirikiana na chama cha soka, FA, kufuta mashindano ya Carabao.
Hii ni kwa sababu ongezeko la timu litamaanisha msimu utakuwa mrefu. Kila timu itacheza mechi 42, kutoka 38 za sasa...hii itafanya ratiba kuwa ngumu kwa kuwepo kwa Carabao.
Hata hivyo, hii itakuwa kwa msimu mmoja tu, wa 2020/21, ambapo mwishoni mwa msimu huo, timu 5 zitashuka daraja ili kurudi kwenye mfumo wa kawaida wa timu 20...na kurudishwa Carabao.
Bahati mbaya ni kwamba vilabu vingi vinapinga kuipa Liverpool ubingwa moja kwa moja...vikitaka msimu ufutwe jumla na kusiwe na bingwa kabisa!
Wakuu wanatarajiwa kukutana Alhamisi ijayo kuamua hatima ya sakata hili pamoja na namna ya kupata timu zitakazoshiriki ligi ya Mabingwa msimu ujao pamoja na Europa League.
Post Comment
No comments