Breaking News

Meshark Elia wa Mazembe afungiwa mwaka mmoja kutojihusisha na soka

Mshambuliaji wa TP Mazembe na DR Congo, Meschack Elia amefungiwa kutojihusisha na masuala yote ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kugushi umri wake ili kupata mkataba wa kucheza Ulaya.

Kufuatia mfululizo wa uchunguzi wa kina uliofanywa na Shirikisho la Soka la DR Congo, imeonekana kuwa Elia alibadilisha mwaka wake wa kuzaliwa katika pasipoti mpya kutoka mwaka wa kuzaliwa 1996 hadi 1997 ili kumuwezesha kujiunga na klabu ya Young Boys ya nchini Uswizi.

Pia mshambuliaji huyo amebainika kwamba alikuwa amesaini mkataba kinyume na utaratibu, kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na TP Mazembe.

No comments