Zidane presha imeshuka

Madrid, Hispania . Mshambuliaji nguli, Karim Benzema amempa raha Zinedine Zidane baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Sevilla.
Nyota huyo wa Ufaransa, alifunga bao hilo kwa kichwa katika mazingira magumu akiwa ndani ya eneo la hatari la wapinzani wao.
Ushindi huo umepoza machungu ya Zidane ambaye alipoteza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya timu yake kulala mabao 3-0 dhidi ya Paris Saint Germain (PSG).
Idadi kubwa ya mashabiki walichukizwa na matokeo hayo, lakini Zidane aliahidi kulipa kisasi dhidi ya Sevilla.

No comments